Mfanyabiashara wa bembejeo za kilimo nchini Tanzania ambaye pia ni mfugaji mkubwa wa Ng’ombe, Gesso Bajuta ameonya dhidi ya hasara kubwa inayoweza kuwapata wafugaji wanaomiliki Ng’ombe wengi kwa mtindo wa kuhama hama, kwani mabadiliko ya hali ya hewa yanayoshuhudiwa ulimwenguni, yanaweza kuwafanya wafugaji hao kupoteza mifugo yao yote.Ametoa tahadhari hiyo Septemba 20, 2025 katika kijiji cha Lemugur, kata ya Mateves Halmashauri ya Arusha, wakati wa hafla ya kukabidhi Ndama kwa vikundi 10 vya wanawake 100 wafugaji wa jamii ya Kimasai, kupitia mpango unaoratibiwa na Kampuni ya Saravu Farm Ltd, wa kuwajengea Wanawake hao uwezo na fikra za ufugaji wa kisasa na wenye faida kwa kumiliki Ng’ombe wachache katika eneo dogo.
BAJUTA: WAFUGAJI WENZANGU TUBADILIKE










Leave a Reply