Paul Makonda Ashinda Kura za Maoni CCM Arusha Mjini

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ameibuka kidedea katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Jimbo la Arusha Mjini, akipata kura 9,056 kati ya kura zote zilizopigwa, sawa na asilimia 97.63. Makonda aliongoza miongoni mwa wagombea saba waliowania nafasi hiyo ya kugombea ubunge kupitia chama hicho, nafasi ambayo awali ilishikiliwa na Mrisho Gambo. Matokeo hayo yalitangazwa leo, Jumatatu ya tarehe 4 Agosti 2025, na Katibu wa CCM Wilaya, ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi, Timothy Sanga.

Katika kura hizo, jumla ya wajumbe 9,276 kati ya 10,186 waliosajiliwa walijitokeza kupiga kura. Wagombea wengine waliokuwa kwenye kinyang’anyiro hicho na kura walizopata ni Mustapha Nassoro (83), Hussein Gonga (46), Ally Babu (28), Aminatha Toure (26), Lwembo Mghweno (16), na Jasper Kishumbua (10). Ushindi huo mkubwa wa Makonda unaashiria uungwaji mkono mkubwa wa kisiasa alionao ndani ya chama hicho katika mkoa wa Arusha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *