Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu yenye makao makuu Arusha, Tanzania imepata Rais mpya ambaye ni Jaji Modibo Sacko kutoka Mali, atakayetumikia nafasi hiyo kwa miaka miwili.
Jaji Sacko amechaguliwa jumatatu Juni 02, 2025 na Majaji wenzake 10 katika makao makuu ya Mahakama hiyo jiji Arusha, kuchukua nafadi ya Jaji Imani Aboud raia wa Tanzania, ambaye amekuwa Rais wa mahakama hiyo kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 2021.
Akizungumza na wana habari baada ya uchaguzi huo, Jaji Imani pamoja na mambo mengine amezitaka nchi wanachama wa mahakama hiyo kutekeleza hukumu na amri zinazotolewa na mahakama hiyo.
Naye Jaji mpya, Modibo Sacko ameahidi kuendelea kusimamia utoaji haki kwa Waafrika wote kutoka nchi wanachama wanaofungua mashauri kwenye mahakama hiyo.
Leave a Reply