TPHPA YANUNUA NDEGE KUDHIBITI NZIGE, KWELEAKWELEA

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), imenunua Ndege ya  kunyunyizia Viuatilifu kwa ajili ya kudhibiti mashambulio ya Wadudu na Ndege waharibifu wa mimea na mazao hususani Nzige, Kwelea Kwelea, nk.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Afya ya Mimea, yaliyofanyika Mei 12, 2025 jijini Arusha, Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Profesa Joseph Ndunguru alisema awali Mamlaka hiyo ililazimika kuomba msaada wa Ndege kutoka Shirika la kupambana na Nzige nchini Kenya, ili kuwezesha kukabiliana na mashambulio ya Nzige na Kwelea kwelea katika baadhi ya maeneo nchini.

Leave a Reply to Aderald Michael Rweikiza Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *