Kiwanja cha ndege cha Arusha, kimepata kibali cha kutua ndege ndogo zinazotoka
nje ya Tanzania, baada ya miaka mingi kutumika kama kiwanja cha ndani.
Awali ndege zote zinazobeba abiria wanaotoka nje kwenda Arusha na wanaotoka
Arusha kwenda nje ya nchi wakiwemo Watalii, walilazimika kutumia uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kwa ajili ya ukaguzi wa nyaraka za
kusafiria na mizigo.
Kwa sasa Kiwanja cha Arusha kimetimiza matakwa yote ya kikanuni na kisheria,
ikiwa ni pamoja na kuwa na Maafisa wa Idara ya Uhamiaji, Maafisa Forodha, nk.
Kampuni ya ndege ya Flightlink, imekuwa ya kwanza kufanya safari ya moja kwa
moja kutoka Kiwanja cha ndege cha Arusha kwenda Nairobi, Kenya na kurudi
Arusha.
Jumatatu Juni 16, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameshuhudia
ndege hiyo ikitua katika kiwanja hicho ikitokea moja kwa moja Nairobi, na
baadaye kuzungumza na Wana Habari.
NDEGE KUTOKA NJE KUTUA ARUSHA AIRPORT

Leave a Reply