Wanawake wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) mkoa wa Arusha, wamefanya maombi maalumu kwa ajili ya kuombea amani ya Tanzania wakati wa uchaguzi Mkuu utakaofanyika jumatano hii Oktoba 29, 2025.
Mgeni rasmi katika maombi hayo alikuwa mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude ambaye amewapongeza wanawake kutoka madhehebu mbalimbali ya dini kwa kuandaa tukio hilo muhimu na lenye manufaa kwa taifa.
Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania (JMAT), Askofu Dkt. Israel Maasa amewahakikishia wananchi kuwa nchi ni shwari hivyo wasiogope kwenda kupiga kura, huku akiwataka kupuuzia vitisho na hofu inayosababishwa na baadhi ya watu kupitia mitandao ya kijamii.










Leave a Reply