Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) kutoka Kenya, David Ole Sankok amezihimiza nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na bara la Afrika kwa ujumla kutumia rasilimali ya madini kuondoa umaskini kwa raia wake.
Akichangia taarifa ya Kamati ya Kilimo, Maliasili na Utalii kuhusu tathmini ya Sera na Sheria zinazosimamia shughuli za Madini katika nchi za EAC, katika mkutano wa kwanza, kikao cha nne cha bunge la tano la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Sankok amesema baadhi ya nchi zimejikuta zikiingia katika migogoro ya wenyewe kwa wenyewe kutokana na kugombania madini badala ya kutumia rasilimali hiyo kuimarisha maisha na ustawi wa watu wake.










Leave a Reply