“HATUJASOMA LAKINI TUNAWEZA KUAJIRI WASOMI”

Vijana wanane katika kata ya Kabanga, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera kupitia kikundi chao kinachojulikana kwa jina ka Kabanga Matunda,  wanaendesha kilimo cha Parachichi katika eneo lenye ukubwa wa ekari 28.

Kupitia kwa Mwenyekiti wa kikundi hicho, Livingstone Samwel wanasema wanaishi maisha mazuri kutokana na kilimo cha Parachichi, na kwamba pamoja na kuwa na elimu ndogo wanao uwezo wa kuwaajiri wasomi wahitimu wa vyuo vikuu.

Kwa kutambua jitihada zao, Halmashauri ya wilaya ya Ngara imewapa mkopo wa shilingi milioni 40 ili wajiimarishe zaidi, na pia kwa kushirikiana na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), imewezesha vijana hao kupatiwa mafunzo na mbinu za kulihudumia zao la Parachichi kwa ufasaha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *