
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR), imeiamuru nchi ya Rwanda kujibu madai ya nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo-DRC katika kipindi cha siku tisini, kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu na mauaji ya kimbari yanayodaiwa kufanywa na nchi ya Rwanda, kwa kushirikiana na Waasi wanaopingana na Serikali ya nchi hiyo.
Hukumu hiyo iliyosomwa na Jaji Rafaa Ben Achour kutoka Tunisia, kwa niaba ya Majaji 11 wa Mahakama hiyo inafuatia madai ya DRC inayoitaka mahakama hiyo kuiamuru Rwanda, kuwajibika moja kwa moja kwa uharibifu uliosababishwa na askari wake kwa kushirikiana na waasi wa M23, ikiwa ni pamoja na vitendo vya ubakaji dhidi ya wanawake, mauaji ya maelfu ya watu, uporaji, na kusababisha matatizo ya kisaikolojia dhidi ya watu wa Congo