WASICHANA WALIOKOSA FURSA YA ELIMU WAWEZESHWA UJUZI

Wanawake na wasichana 720 kutoka maeneo mbalimbali nchini, wamenufaika na mpango wa uwezeshaji kupitia ujuzi (ESP), kwa kujifunza program za muda mfupi za kijinsia, Upishi na Tehama zitakazowawezesha kujikwamua kiuchumi. Katika kikao cha maendeleo kupitia program ya ESP kilichofanyika jijini Arusha, na kuwashirikisha Watendaji wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Elimu, Dkt Charles Mahera, pamoja na Serikali ya Canada inayofadhili mpango huo, iliyowakilishwa Bi Carol Mundle, ambaye ni Kansela Mkuu, Ushirikiano na Maendeleo katika Ubalozi wa Canada nchini Tanzania, kwa pamoja wameahidi kuendeleza ushirikiano kuhakikisha vijana hususani wasichana waliokatiza masomo yao, wanatimiza ndoto zao kwa kupatiwa mafunzo mbalimabali, kupitia Vyuo 12 vya Maendeleo ya Wananchi kati ya 54 vilivyopo nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *